- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MTANZANIA AWA BILIONEA SIKU MOJA KWA KUPATA ALMASI YA BILIONI 3
Shinyanga: Maisha yamekuwa tofauti kwa mtanzania Joseph Temba ambae ni mchimbaji mdogo wa madini wa mkoani Shinyanga baada ya kuwa Tajiri ghafla kwa kuuza almasi yake kwa takriban dola za kimarekani milioni moja nukta nne($1.4m) sawa na Shilingi Bilioni 3.
Inataarifiwa kuwa Almasi hiyo yenye karati 512 ilipatikana na mchimbaji madini huyo wiki mbili zilizopita katika eneo la Maganzo huko mkoani Shinyanga.
Bwana Temba ameishukuru Wizara ya Madini na Tume ya Madini kwa muongozo na usimamizi wa Almasi yake na muongozo wa utaratibu wa mauzo ambao uko wazi.
Kulingana na naibu waziri wa madini nchini humo Stanlaus Nyongo almasi hiyo ndio kubwa zaidi kuwahi kupatikana nchini humo.
Naibu Waziri Nyongo alishuhudia uuzwaji wa almasi hiyo na kusema kuwa Serikali yapata Milioni 238 kutokana na mauzo hayo.
Nyongo amewahimiza na kuwasisitizia wachimbaji wote na wanunuzi kote nchini kufanya shughuli hizo kwenye masoko ya madini yaliyoainishwa na kutambulika na Serikali.