- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MSEMAJI MKUU WA RAIS WA MAREKANI BW TRUMP AMEJIUZULU WAZIFA WAKE
New York: Msemaji mkuu wa Rais wa Marekani Sean Spicer amejiuzulu wazifa wake kama msemaji mkuu wa whitehouse taarifai zinasema kuwa Spicer aliamua kujiuzulu kwa sababu hakufurahishwa na uamuzi wa rais Trump kumteua Mkurugenzi mpya wa mawasiliano katika mpangilio mpya katika idara ya Mawasiliano.
Ripoti zinasema kuwa Anthony Scaramucci mfadhili wa kampuni ya Wall Street ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa mawasiliano katika Ikulu hiyo.
Spicer mwenye umri wa miaka 45, amesema amemwambia Trump kuwa anaamini kuwa kuwepo kwa Mkurugenzi wa mawasiliano kutatiza kazi yake katika Ikulu ya White House.
Amefananisha mabadiliko hayo kama kuwa na wapishi wengi jikoni ambao amesema wanaweza kuharibu mapishi.Msemaji huyo wa zamani amekuwa akimtetea rais Trump na kuvishtumu vyombo vya Habari nchini humo kuwapotosha Wamarekani kuhusu uongozi wa Trump.
Trump amemshukuru Spicer kwa kazi aliyoifanya na hasa kumtetea mbele ya wanahabari nchini humo hasa kuhusu madai ya Urusi kuingilia Uchaguzi wa Marekani mwaka uliopita.
Kujiuzulu kwa Spicer kunakuja wakati huu bunge la Senate likiendelea kuchunguza madai ya Urusi kuingilia Uchaguzi huo lakini pia likiwahoji washirika wa karibu wa rais Trump akiwemo Mwanasheria Mkuu wa serikali Jeff Sessions.