- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MSANII BABA LEVO ASHINDA RUFAA YAKE
Msanii wa Bongo Fleva na Diwani wa kata ya Mwanga Kaskazini, kupitia chama cha ACT Wazalendo Manispaa ya Kigoma Ujiji, Clyaton Revocatus Chipando maarufu Baba Levo leo Novemba 21, 2019 ameshinda Rufaa yake katika Mahakama kuu Mkoa wa Kigoma.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kigoma ilimuongezea kifungo kutoka miezi 5 aliyopewa awali na mahakama ya Mwanzo ya Mwandiga hadi mwaka mmoja
Hukumu hiyo ilitolewa mnamo Septemba 10, 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, baaada ya kushindwa rufaa yake ya kupinga hukumu ya awali.
Baba Levo alikata rufaa katika mahakama hiyo kupinga adhabu ya awali ya miezi mitano, kwa kosa la kumshambulia trafiki, F.8350 PC Msafiri Mponela.
Katika hukumu ya awali Baba Levo alitiwa hatiani kwa kifungu namba 240 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 chapisho la mwaka 2002 na hukumu yake kutolewa Alhamisi Agosti 1, 2019, katika mahakama ya Mwanzo Mwandiga na Hakimu Mkazi Florence Ikolongo.