- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MSAJILI WA NGOs ATOA SIKU 7 KWA MASHIRIKA YASIYOHUISHA TAARIFA ZAKE
DODOMA: Ofisi ya msajili wa Mashirika yasiyo ya kiserikali(NGOs) imeongeza muda wa wiki moja kwa mashirika yasiyohuisha taarifa zake kuweza kufanya hivyo la sivyo yatakuwa yamejiondoa kwenye rejista ya msajili.
Zoezi hilo linawahusu wanaohama kutoka kwenye sheria mbalimbali walizosajili awali kama sheria ya makampuni,wadhamini na sheria ya jumuiya na kuhamia katika sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali namba 24 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa chini ya sheria namba 3 ya mwaka 2019.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake msajili wa NGOs Vickness Mayao amesema hatua hiyo inafanyika kufuatia kupitishwa kwa marekebisho ya usajili wa NGO’s.
Mayao amesema zoezi hilo la usajili lilishafanyika katika kanda tano ambazo ni kanda ya Mashariki,Kanda ya Kati,Kanda ya Kaskazini,Kanda ya Ziwa na kumalizia Kanda za nyanda za juu kusini ambapo limefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 85.
Mafanikio mbalimbali yanatajwa kupatikana baada ya zoezi la usajili ikiwemo wananchi wamekuwa na imani kuhusu nia njema ya serikali katika dhamira yake ya mabadiliko ya sheria ya NGO’s,huduma za usajili zimekuwa ni rahisi na rafiki na hofu iliyokuwepo kuhusu ujio wa mabadiliko ya sheria hiyo mpya imetoweka na kuna ushirikiano mkubwa kati ya wadau na serikali.