- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MSAIDIZI WA ZITTO BW. RAPHAEL APATIKANA AKIWA HAI
Mfanyabiashara wa Kenya na msaidizi wa Mbunge wa Upinzani nchi Tanzania Zitto Kabwe Bw. Raphael Ongangi aliyetekwa nyara hapa nchini kutokana na madai ya kisiasa amepatikana mjini Mombasa mchana wa leo Jumanne.
Raphael Ongangi alitekwa Jumatatu usiku katika viunga vya mitaa ya Oysterbay jijini Dar es Salaam na watu wenye silaha akiwa na mke wake Veronica Kundya.
Mkewe Veronica amethibitisha kupatikana kwa mumewe mapema leo siku ya Jumanne.
''Nimezungumza naye mwenyewe yupo Momabasa , tumezungumza kwa ufupi anashukuru sana'', amesema Veronica
Mwanaharakati wa haki za kibinaadamu nchini Kenya Boniface Mwangi ametuma ujumbe wa Twitter akisema kuwa Mfanyabiashara huyo ambaye kwasasa anadaiwa kulazwa katika hospitali ya Aga Khan mjini Mombasa alitupwa mjini humo na maafisa wa ujasusi.
Mwamngi amewashukuru wote waliohusika katika kampeni iliosababisha kuachiliwa kwake.
, watu wasiojulikana waliwafuatilia wanandoa hao na kisha kulizuia gari yao na kumchukua bwana huyo na kuondoka naye.
Awali bi Veronica anasema aliamriwa na watu hao ambao anadai walijatambulisha kama maafisa wa usalama kuwa asiseme chochote mpaka atakapotaarifiwa nao.
Na baada ya takribani saa moja akapokea simu kutoka kwa mumewe iliyomtaka kurejea nyumbani na wala asiripoti tukio hilo mahali popote.
Taarifa zilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii zinaripoti kuwa Ongangi aliingia Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 2000 kwa masomo ya elimu ya juu katika moja ya vyuo vikuu nchini humo.