- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MRUDIKANO WA WANAFUNZI MADARASANI BADO NI KIKWAZO NCHINI.
DODOMA: Wadau wa elimu ya awali nchini wamesema mrudindikano wa wanafunzi wa darasa la awali umekuwa kikwazo kwa wanafunzi wa darasa hilo hali inayowafanya walimu kushindwa kumfikia mwanafunzi mmoja mmoja katika ufundishaji.
Wameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa mkutano uliowaandaliwa na serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Tekonolojia pamoja na Tamisemi ukiwashirikisha wadau mbalimbali wa elimu ya awali wakiwemo asasi za kiraia, vyuo vikuu na waalimu.
Mmoja wa wachangiaji katika mkutano huo, Mwalimu wa darasa hilo katika shule ya msingi Madizini wilayani Mvomero Mkoani Morogoro Monica Kibena alisema, madarasa wanayofundisha yana wanafunzi kuanzia wanafunzi 150 hadi 200 ambao alisema ni mwalimu mmoja hawezi kulimudu darasa .
Kibena alisema,mrundikano huo unawafanya walimu kushindwa kufanya upimaji wa mtoto mmoja mmoja ili kujua uelewa, hivyo ili kuikabili changamoto ni vyema Serikali ijenge madarasa ya kutosha na kuwagawangwa wanafunzi hao kwa uwiano unaotakiwa wa wanafunzi 25 kwa mwalimu mmoja.
“Kwa kweli mrundikano wa wanafunzi wa darasa la awali bado ni changamoto kubwa kwetu,wanafunzi wengi sana hatua inayowafanya walimu wengi kushindwa kulimudu darasa kwa wanafunzi wa darasa hilo wanapaswa kufikiwa mmoja mmoja ili kujua uelewa wake kwani ndio msingi wake
Mwalimu Kibena alitumia fursa hiyo pia kuishauri Serikali kuwatumia baadhi ya walimu waliopata mafunzo akiwemo yeye kutoka CIC ambayo yamewezesha kulimudu darasa kubwa .
Aidha Mwalimu Kibena amewataka walimu wenzake kuwa wabunifu kwa kutafuta zana za kufundishia kulingana na mazingira ili kuongeza uelewa wa wanafunzi wanapokuwa shuleni.
Awali Mkurugenzi Mkazi wa shirika linaloshughulika na masuala ya makuzi na malezi ya awali ya watoto wadogo (CIC) Craig Ferla amesema kuwa wadau wa elimu wanapaswa kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto za elimu ya awali nchini kulingana na ongezeko la watoto hao.
Bw.Ferla amesema kuwa uandikishaji wa watoto kwa mwaka 2016 umeongezeka hadi kufikia 1.5 milioni kutoka watoto milioni moja mwaka 2015.
“Zipo changamoto nyingi katika elimu inayotolewa nchini ikiwemo ya awali hasa katika madarasa hayatoshi hivyo kusababisha kuwepo kwa mlundikano wa wafanzi, ili kukabiliana nayo ni lazima wadau wote wa elimu washiriki na si kuiachia serikali peke yake,” amesisitiza Ferla.
Hata hivyo amesema katika kuunga mkono juhudi za serikali kwenye utoaji wa elimu bora nchini wamejipanga kuzindua mradi wa elimu ya awali katika mkoa wa Dodoma mwaka 2020 ambao utatekelezwa katika Wilaya ya Kongwa pamoja na Chamwino na baadae kuenea mkoa katika halmshauri zote saba zilizopo mkoani humo .
Amesema mradi huo unalenga kujenga uwezo wa watendaji wakiwemo waalimu wanaofundisha elimu ya awali, wathibiti wa ubora na maofisa elimu katika wilaya za mkoa husika.
Akifungua Kikao hicho kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Elimu Avemaria Semakafu, Mkurugenzi Msaidizi Uendeshaji wa Sera wa wizara hiyo Bw.Yesse Kanyuma aliipongeza Asasi ya CIC kwa kuanzisha mradi huo ambao unawajengea watoto umahiri pamoja na kutoa mbinu za ufundishaji wa watoto wa darasa la awali.
“Nimeambiwa kuwa shirika hili limekuwa likitekelza programu za watoto hapa nchini kwa ufanisi tangu mwaka 2009 katika mikoa ya Kilimanjaro ,Mwanza na Morogoro .