- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MRITHI WA TUNDU LISSU ALA KIAPO LEO BUNGENI AKISUBIRI SEPTEMBA 9
Spika wa Bunge la TanzaniaJob Ndugai leo Jumanne amemuapisha Mbunge wa Mteule wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu, kutoka chama cha ccm Bungeni jijini Dodoma, akirithi nafasi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Tundu Lissu, ambaye alivuliwa Ubunge na Spika wa Bunge Job Ndugai mnamo Juni 28 mwaka huu.
Tundu Lissu amekuwa nchini Ubelgiji akipokea matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mchana wa Septemba 7 mwaka 2017.
Lakini wakati akiwa huko Spika Ndugai alimvua ubunge kwa madai kwamba hakuwa ametoa taarifa rasmi ya alipo, na pia hakuwa amejaza fomu za mali na madeni ya viongozi wa umma.
Mtaturu alitangazwa mbunge mteule wa jimbo hilo kwa kupita bila ya kupingwa katika hatua za awali za matayarisho ya uchaguzi mdogo baada ya wagombea 12 wa vyama vya upinzani kutorejesha fomu.
Uchaguzi huo mdogo ulikuwa ufanyike Julai 31, lakini haukufanyika tena kutokana na wapinzani kutokurejesha fomu zao.
Hata hivyo, kuna kesi mahakamani ambayo inaweza kuathiri kiapo cha Mtaturu hii leo pale ambapo maamuzi yake yatakapotolewa wiki ijayo.
Kesi hiyo imepelekwa mahakamani na Lissu akipinga kuvuliwa ubunge wake.
Jana Katika mahakama kuu jijini Dar es salaam mawakili wa Lissu walitarajia kuzuia kuapishwa kwa Mtaturu hii leo hadi pale kesi hiyo itakaposikizwa na kuamuliwa.
Hata hivyo, Jaji Sirillius Matupa wa Mahakama Kuu ya Tanzania alilikataa ombi hilo la mawakili wa Lissu akisema katika kesi za ubunge hata kama mtu ameapishwa anaweza kuvuliwa ubunge pamoja na kiapo chake.
Kesi hiyo hapo jana iliunguuma mpaka saa tatu kasoro robo usiku ambapo Jaji alitangaza maamuzi yake juu ya ombi la kiapo cha Mtaturu.
Jaji Matupa amesema kuhusu maombi rasmi ya Lissu kupinga kuondolewa katika ubunge yatatolewa Septemba 9, 2019.