- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MREMA AVURUGWA APANGA KUMSHTAKI RAIS MAGUFULI
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema ameitaka Serikali ya Tanzania chini ya Rais Magufuli kumlipa Shiling bilioni 2 kama fidia ya kesi alizowahi kusingiziwa chini ya Serikali ya awamu ya tatu ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Mrema amesema amemuandikia barua Rais wa Tanzania, John Magufuli yenye malalamiko yake na kuomba kukutana naye ili waweze kuzungumza juu ya yale aliyofanyiwa na serikali ya CCM.
Kauli hiyo ya Mrema ameitoa leo Jumatano Januari 8, 2020 katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya TLP, Magomeni jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia hali ya kisiasa nchini tangu awamu ya tatu hadi sasa.
Amesema kwa nyakati tofauti ndani ya uongozi wa Rais Mkapa alisingiziwa kesi ikiwamo ya kumhusisha Rais huyo na rushwa ya Sh500 milioni akiwa katika kampeni za kugombea ubunge wa Temeke mwaka 1996, kutengeneza nyaraka mbalimbali zilizohusisha viongozi wa serikali na tuhuma za rushwa pamoja na kutumia ushahidi wa uongo kushinda kesi.
Amesema kwa sababu Serikali imesema kumbambikia kesi mtu ni kosa la jinai ambapo wahusika wanatakiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani lakini muathirika anatakiwa kulipwa fidia ameomba Rais Magufuli kumlipa fidia kwa niaba ya serikali.
Kwa kuwa nilibambikiwa na kuzushiwa ya uongo ambayo ni kosa kisheria, nakuomba Rais wa Tanzania (John Magufuli) na serikali yako inilipe Sh2 bilioni kwani haya yote yalifanyika ili kukisaidia chama tawala na serikali yake ili kinishinde kisiasa,” amesema Mrema
“Hiyo hela ni ya chumvi na wasiponifidia nitawashtaki kwa wananchi na ninamuomba Rais Magufuli afute historia ya kuonewa kwa watu nchini na kuonewa kwangu,” amesema
Amesema kitendo cha kupewa kesi za uongo kulimuathiri kisaikolojia kwani jamii iliyokuwa ikimzunguka ilimuona kama mtu mwovu kutokana na kukamatwa na polisi kila mara.
“Sioni unafuu katika kunyamaza kwa sababu nchi hii ukiwa na nguvu wanaangalia namna ya kukudhoofisha kwa kutumia mbinu tofauti na hila kwa kutumia vyombo vyao,” amesema Mrema
“Mengine nimevumilia sana mpaka basi, wapo wengine wanasema hakuna wa kuiondoa CCM madarakani ni kweli, inaondokaje kwa udhalimu huu na mtaji iliyonayo,” amesema Mrema