- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MPINA AWAPIGA NYUNDO NZITO WANAOKULA NJAMA KUMHUJUMU MAGUFULI.
MWANZA: Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM) Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina amewashukia baadhi ya watu waliowahi kupewa nyadhifa za juu serikalini na kwenye Chama cha Mapinduzi kuendesha mikakati na kula njama za kutaka kumuondoa Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye ajenda kuu ya kuwahudumia wananchi na kutaka taifa lijadili mambo ya watu binafsi.
Akizungumza na maelfu ya wananchi wa Jimbo la Kisesa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Malwilo Kata ya Tindabuligi na kuhudhuriwa na wananchi wote wa jimbo hilo, Mpina ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi amesema watanzania wanaimani kubwa na Serikali ya awamu ya tano na kwamba mikakati na njama hizo kamwe hazitafanikiwa.
Mpina amesema viongozi hao hao waliowahi kupewa nafasi za juu ndani ya CCM na Serikali lakini watanzania walishuhudia usimamizi dhaifu wa shughuli za chama na kusababisha makundi makubwa ya viongozi na wanachama kuhamia vyama vya upinzani na kuisababishia CCM na Serikali kuchukiwa na wananchi.
Mpina amesema baada ya Mwenyekiti wa CCM na Rais Dk. Magufuli kufanikiwa kusuka upya mifumo, kufumua mikataba na sheria mbalimbali na kuongeza udhibiti na usimamizi wa rasilimali za nchi pamoja na kupambana na rushwa kwa vitendo na kukomesha mambo machafu yaliyokuwa yanaumiza wananchi ndio wanaibuka watu wachache kutoa waraka na kutaka kuwahamisha wananchi kwenye ajenda kuu ya maendeleo ili wajadili mambo binafsi kwa masilahi yao.