- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MOURINHO AHUKUMIWA MWAKA 1 KWENDA JELA
Kocha wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwenda Jela au kulipa faini ya Euro milioni 2 kwa kosa la ukwepaji kodi nchini Uhispania wakati akiwa kocha wa Real Madrid.
Mourinho amekiri makosa yake, anatarajiwa kulipa faini ya Euro 182,500 (£160,160) kama malipo ya awali katika faini yake ya Euro milioni 2.
Uhispania hata hivyo huwa haiwafungi jela wahalifu ambao wamehukumiwa kifungo cha chini ya miaka miwili na wale ambao hawajatumia mabavu kwenye kutenda uhalifu wao.
Wendesha mashtaka walimtuhumu kocha huyo kukwepa kodi ya Euro milioni 3.3m (£2.9m) katika kipindi ambacho alikinoa kikosi cha Real Madrid Real Madrid kati ya 2011-2012.
Mourinho anatuhumiwa kuanzisha makampuni kadhaa visiwani British Virgin Islands ili kusimamia mapato yake yatokanayo na picha.
Waendesha mashtaka wanadai kuwa makampuni hayo yaliundwa ili kuficha mapato halisi ya mkufunzi huyo na kuathiri kiasi cha kodi alichotakiwa kulipa.
Makubaliano ya adhabu hiyo yalifikiwa na Mourinho na maafisa kodi hapo awali, na leo walienda mahakamani ili kuyapa uhalali wa kisheria.