November 27, 2024, 3:29 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MOTO WATEKETEZA NYUMBA 13 ZA ASKARI POLISI
Arusha: Familia 13 zenye zaidi ya watu takribani 44 zimeteketea kwa moto ulioibuka kwenye nyumba za askari polisi usiku wa kuamkia leo katika Kata ya Sekei mkoani Arusha.
Taarifa za awali za mashuhuda zinasema kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme na polisi wanaendelea na uchunguzi kujua ukweli huo.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho gabo amesema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo.Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoani Arusha, Andrew Komba amesema moto huo ulidhibitiwa muda mchache baadae.
“kama Tungefika mapema nusu ya nyumba zilizoteketea tungeziokoa,” amesema Komba.
Amesema taarifa kuhusu tukio hilo zimewafikia kwa kuchelewa.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema hali ni shwari na hakuna wizi uliotokea.
Amesema tukio hilo ni janga, hivyo watakaa kuona ni kwa namna gani watawasaidia walioathiriwa