Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:44 pm

NEWS: MORSI AZIKWA HARAKA NA KIMYA CHINI YA ULINZI MKALI

Rais wa kwanza wa Misri aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia Mohammed Morsi amezikwa leo, huku miito ikizidi kuongezeka ya kutaka kufanyike uchunguzi huru juu ya sababu za kifo chake baada ya kuanguka katika chumba cha mahakama mjini Cairo.

Image result for mohamed morsi death

Mmoja wa wanasheria wake amesema kiongozi huyo wa zamani kutoka kundi la Udugu wa Kiislamu, aliyeondolewa madarakani mwaka 2013 baada ya mwaka mmoja wa utawala uliokuwa na mgawanyiko na baadaye kukabiliwa na mashtaka ya ujasusi, alizikwa katika eneo la makaburi la Medinat Nasr kusini mwa mji wa Cairo.

Mnamo mwezi Machi 2018, kundi la wabunge wa Uingereza lilionya kwamba hali yake ya kuwekwa kizuizini haikufikia kiwango cha kimataifa na huenda ingelimsababishia kifo cha mapema.

Image result for mohamed morsi cemetery foundInasemekana hili ndio eneo alilozikwa Morsi

Wanachama wengine wa kundi la Udugu wa Kiislamu pia walifariki wakiwa kizuizini. Washirika wake kama vile Qatar na Uturuki wametuma salamu za rambirambi, huku wizara ya mambo ya nje ya Iran ikisema kifo cha Morsi kinahuzunisha na ni cha bahati mbaya. Kimataifa kuna waliomuunga mkono Morsi, lakini nchini Misri ameacha historia yenye mitazamo ya mchanganyiko.