- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MOISE KATUMBI AAHIDI KURUDI CONGO MAY 20
Moise Katumbi , mfanyabiashara tajiri na gavana wa zamani wa jimbo la Katanga ametangaza kwamba baada ya miaka mitatu akiwa uhamishoni, anatarajia kurudi kwa ndege Lubumbashi Mei 20. Katumbi alizuiliwa kuingia nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kushitakiwa kwa makosa dhidi ya usalama wa taifa. Katumbi mwenye umri wa miaka 53, anaishi uhamishoni nchini Ubelgiji tangu Mei 2016 baada ya kutofautiana na rais Joseph Kabila, ambaye ameitawala DRC kwa miaka 17.
Tangu uchaguzi wa urais Desemba 30, kiongozi huyu wa upinzani nchini DRC, alikuwa akiishi uhamishoni.
Hivi karibuni vyombo vya sheria vya DRC vilimsafisha Moise Katumbi kwa makosa mawili yaliyokuwa yakimkabili katika kesi ya madai ya udanganyifu wa mali.
Pia alikuwa anashutumiwa kwa kukodi mamluki na kuwa na pasi ya kusafiria ya italia, ambapo sheria za Congo haziruhusu mtu kuwa na uraia pacha wa mataifa mawili.
Moise Katumbi amepongeza vyombo vya sheria vya DRC kwa hatua hiyo na kusema ana furaha ya kurejea nchini.
Kiongozi huyo wa upinzani alikataliwa kuingia DRC kupitia mpaka na Zambia wakati alipojaribu kurejea kutoka uhamishoni ili kuwasilisha fomu yake ya kuwania urais katika uchaguzi wa mwezi Desemba.
Katumbi alikuwa anatakabiliwa na kukamatwa baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela wakati akiwa hayupo mahakamani mwezi Juni 201