Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 1:18 am

NEWS: MOI YAFANIKIWA KUFANYA UPASUAJI CHINI YA FUVU LA KICHWA

Madaktari Bingwa wa Upasuaji ubongo wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), wamefanikiwa kwa mara ya kwanza kufanya upasuaji mgumu wa kuondoa uvimbe uliokuwa chini ya fuvu la kichwa kwa kutumia darubini ya kisasa.

“Tumefanikiwa kufanya upasuaji huo kwa kushirikiana na mabingwa wenzao kutoka Hospitali ya Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha nchini China.

“Tumepokea jopo la mabingwa watatu, ushirikiano wetu ni wenye manufaa makubwa kwani huduma za MOI zitaendelea kuwa bora na watanzania wataendelea kupata huduma hizo hapa nchini billa ya kwenda nje ya nchi" alisema jana Daktari Bingwa wa Upasuaji Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu MOI, Nicephorus Rutabasibwa wakati akizungumza na wanahabari.

Rutabasibwa alisema upasuaji huo ni mgumu na huchukua muda mrefu kukamilika.

“huu ni muendelezo wa ushirikiano tulioingia na wenzetu hawa wa Peking mwaka jana, tunaamini tutabadilishana uzoefu na wenzetu hawa ambao wamepiga hatua kubwa kwenye teknolojia ya matibabu, kupitaia ushirikiano huu mbinu tunazopata zitatusaidia kuendelea kutoa tiba bora na kwa wakati kwa wagonjwa wetu” alisema.