- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MNYIKA AORODHESHA VIPAUMBELE VYAKE KUELEKEA UCHAGUZI 2020
Dar es Salaam. Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika ameorodhesha vipaumbele vyake vikuu vitano vya chama hicho katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Mnyika ambaye kwasasa pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibamba ameeleza hayo leo Jumapili Desemba 22, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Amevitaji kuwa vipaumbele hivyo ni kudai tume huru ya uchaguzi, maandalizi ya wagombea kuelekea uchaguzi mkuu, ilani ya uchaguzi ya chama hicho na kuendeleza sera ya Chadema msingi na Chadema Digital.
"Mosi, kudai Tume Huru ya Uchaguzi kama ilivyoazimiwa na mkutano mkuu, Baraza Kuu na Kamati Kuu kwa kuzingatia kuwa chaguzi ndogo zilizosimamiwa Tume ya Uchaguzi (NEC) na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa zilizosimamiwa na Tamisemi zote hazikuwa huru wala za haki"
Mnyika aliyeteuliwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuwa katibu mkuu Desemba 20, 2019 kuchukua nafasi ya Dk Vicent Mashinji amewashukuru wanachama waliopokea vyema uteuzi wake, mbunge huyo wa Kibamba amesema, “kazi kubwa ya chama cha siasa ni kushika dola, hili ndio lipo mbele yetu kwenye uchaguzi wa mwakani.
"Katika mkakati huu tumekuja na vipaumbele hivi vitano ambavyo vikitekelezwa kwa ufanisi Watanzania watarajie mabadiliko.”
Aidha Katibu Mkuu huyo ametumia mkutano huo kumtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro kueleza alipo ofisa wa kitengo cha elimu kwa umma wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti anayeshikiliwa na polisi. Licha ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kusema kuwa polisi wanamshikilia ofisa huyo, hajasema anashikiliwa kituo gani jambo linalolalamikiwa na uongozi wa kituo hicho.