Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 1:24 am

NEWS: MMILIKI WA TIP MAZEMBE AMTAKA RAIS KABILA KUONDOKA MADARAKANI MAPEMA

Congo: Mmiliki wa klabu ya Tip mazembe na Gavana wa zamani wa Jimbo la Katanga nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Moise Katumbi Chapwe, amesema ataitisha maandamano ikiwa Rais Joseph Kabila atashindwa kuandaa uchaguzi mkuu na kuachia madaraka ifikapo Disemba 31, mwaka huu.

Akihojiwa na kituo cha habari cha Ufaransa cha France 24, Katumbi amesema ikiwa rais Joseph Kabila hataitisha uchaguzi mkuu, upinzani utatumia ibara ya 64 ya katiba ya Congo kuwaambia wananchi wamshinikize kuondoka madarakani kabla ya December 30 2017

Moise Katumbi, aliwahi kuwa rafiki wa zamani wa Rais Joseph Kabila, kwa sasa anaishi uhamishoni katika nchi za Ufaransa na Ubelgiji tangu alipotofautiana na Kabila mwaka 2015 na mahakama nchini DR Congo ilimhukumu kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la uporaji wa nyumba ya raia mmoja wa kigeni.

Kiongozi huyo amesema anapanga kurejea nchini mwake ili kuendelea na harakati za kisiasa.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inakabiliwa na mgogoro wa kisiasa baada ya rais Kabila kushindwa kuondoka madarakani licha ya kumalizika kwa muda wake Disemba mwaka 2016 hatua iliyolazimisha kusainiwa kwa makubaliano yanayotaka uchaguzi ufanyike kabla ya Disemba 31 mwaka huu.