- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MMILIKI MAGARI YA MASHALLAH MBARONI KWA KUUZA DAWA ZA KULEVYA
Dar es salaam: MFANYABISHARA mkubwa jijini Dar es salaam ambae ndio mmiliki wa magari ya biashara yaliyoandikwa Mashallah anashikiliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa tuhuma za kujihusisha na kusafirisha dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa Mamlaka hiyo, ni kwamba mfanyabishara huyo aliyetambuliwa kwa jina la Abuu Kimboko amekuwa akitafutwa na nchi mbalimbali kutokana na tuhuma za kujihusisha na biashara hiyo na hatimate amenazwa na sasa.
Anashikiliwa na vyombo vya ulinzi na usalama wakati taratibu za kupelekwa mahakamani zikiandaliwa ili sheria ichukue mkondo wake.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya James Kaji akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kukamatwa kwa watu wawili akiwemo mfanyabishara mkubwa jijini Dar Abuu Kimboko ambao wanatuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Kamishna wa Sheria wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Burhani Kishenyi(katikati) akifafanua masuala ya kisheria katika utendaji wao wa kazi za kukabiliana na dawa za kulevya nchini.