Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:29 am

NEWS: MKUU WA MKOA IRINGA HAPI ASITISHA UTOAJI LESENI KWA WAGANGA WA JADI

Iringa: Mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi amesitisha utaratibu wa Utoaji Leseni kwa waganga wa Jadi Mkoani Iringa kutokana na Mkoa huo Kugubikwa na Wimbi kubwa la ubakaji, ulawiti wa watoto unao husishwa na Pombe na Ushirikina.

Hapi amesema kuwa Mkoa wa Iringa kwa sasa Unawaganga waliosajiliwa na Kupewa leseni wapatao 878 huku wanganga zaidi ya 500 hawana Leseni

Kupitia taarifa aliyoitoa leo siku ya Jumanne jioni Feb 19, 2019 kwenye Ukurasa wake wa Twitter Hapi amesema amesitisha pia Unywaji wa pombe kwa nyakati za kazi.

" Nimesitisha utoaji leseni kupisha uhakiki,kuzuia pombe saa za kazi na tumeanza kura ya siri ya jamii."

Watoto takribani 10 wameshauawa toka visa hivyo vya kikatili kuanza kuripotiwa mwezi Disemba.

Miili ya watoto hao imekutwa ikiwa imenyofolewa baadhi ya viungo kama matumbo, vidole, pua na macho. Wauaji hao pia wamekuwa wakinyofoa viungo vya siri vya watoto hao.

Februari 12, 2019 Washukiwa watatu wa utekaji na mauaji ya watoto wa chini ya miaka 10 wilayani Njombe, kusini magharibi mwa Tanzania wamepandishwa mahakamani.

Watuhumiwa hao waliowekwa wazi kwa mara ya kwanza ni Nasson Kaduma, Joel Nziku na Alphonce Danda.