Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 10:37 am

NEWS: MKUU WA MAJESHI WA ETHIOPIA APIGWA RISASI

BreakingNews: Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ametoa taarifa kuwa mkuu wa majeshi wa nchi hiyo Jenereali Seare Mekonen amepigwa risasi baada ya kuzuka machafuko jana Jumamosi jioni baada ya kutokea kwa jaribio la mapinduzi katika jimbo la Amhara. Hata hivyo hali ya mkuu huyo wa jeshi haijulikani.

Image result for Seare Mekonen shooting

Kwa mujibu wa mwandishi wa shirika la habari la AFP, Rais Abiy alizungumza kupitia kwenye televisheni ya taifa akiwa amevaa mavazi rasmi ya kijeshi baada ya kutokea jaribio la mapinduzi katika jimbo la Amhara lakini maelezo zaidi hayakutolewa kuhusiana na lengo la mashambulio hayo katika jimbo la pili lenye watu wengi zaidi nchini Ethiopia linaloongozwa na Rais wa kikanda Ambachew Mekonen.

Ubalozi wa Marekani ulitoa tahadhari baada ya kusisikia milio ya bunduki katika mji mkuu wa Addis Ababa, na pia vurugu karibu na mji mkuu wa jimbo la Amhara, Bahir Dar.

Image result for Seare Mekonen shooting

Serikali ya Ethiopia imesema jaribio hilo la kuipindua serikali ya kikanda kaskazini mwa nchi hiyo lilishindikana. Ofisi ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed imelaani jaribio hilo la mapinduzi katika ujumbe wa Twitter uliochapishwa Jumamosi jioni.

Wakazi katika mji mkuu wa mkoa huo, Bahir Dar, wameripoti kusikia milio ya bunduki. Nchini Ethiopia mara nyingi mivutano ya kikabila imekuwa ndio chanzo cha mapigano katika nchi hiyo ambayo kwa muda mrefu imetawaliwa kwa mkono wa chuma.

Tangu Abiy alipochukua mamlaka mwezi wa Aprili 2018, ameleta mageuzi, ikiwa ni pamoja na kuwaachia wafungwa wa kisiasa, mageuzi ya kiuchumi, ameruhusu makundi ya watu mbali mbali kurudi nchini, na ameaahidi kupambana na vitendo vinavyokiuka haki za binadamu na amejaribu kuboresha uhuru wa vyombo vya habari.

Lakini Wasziri Mkuu Abiy Ahmed anakabiliana na kuongezeka kwa mivutano kati ya makundi ya kikabila katika nchi hiyo ambayo kwa kawaida ni juu ya ardhi na rasilimali, mivutano hiyo inasababisha vurugu mbaya katika nchi yenye watu zaidi ya milioni 100.