- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MKUU WA MAJESHI NCHINI CONGO AUWAWA NYUMBANI KWAKE
Naibu mkuu wa majeshi ya FARDC, Nchini DRC Congo ambaye pia ni Mkuu wa idara ya ujasusi katika jeshi la Congo Jenerali Delphin Kahimbi amekutwa amefariki dunia nyumbani kwake jijini Kinshasa leo Ijumaa.
Habari hiyo imetolewa na mkewe na washirika wenzake kadhaa wa karibu. Uchunguzi unaendelea, afisa mmoja wa jeshi amebaini. Jenerali Delphin Kahimbi aliitwa mara kadhaa katika siku za hivi karibuni kujibu tuhuma zinazomkabili (uhusiano na makundi yenye silaha na kujaribu kuhatarisha usalama).
Kulingana na vyanzo kutoka ikulu ya rais, Jenerali Delphin Kahimbi alikuwa amesimamishwa kazi.
Msemaji wa jeshi amekiri kwamba uchunguzi umeanzishwa ili kubaini sababu za kifo chake.
Kifo chake kinakuja baada ya kusimamishwa kazi tu.Hii ni habari mbaya sana kwa DRC. Ijumaa hii asubuhi, Mkuu wa idara ya ujasusi katika jeshi, Jenerali Delphin Kahimbi, amefariki dunia katika hospitali ya Cinquantaire jijini Kinshasa, kwa mujibu wa chanzo ambacho hakikutaka jina lake litajwe.
Jenerali Delphin Kahimbi, ambaye alikuwa anakabiliwa na vikwazo vya Ulaya na Marekani tangu 2016, anatuhumiwa makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini DRC.