Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 7:30 pm

NEWS: MKUU WA MAJESHI AWATAHADHARISHA WANAOTOA KAULI ZA UCHOCHOZI

Dadoma: Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo amesema wao kama jeshi linaendelea kufuatilia kauli tata zinazoashiria uchochezi na kuhatarisha kuibua machafuko ndani ya nchi, ameongezea kuwa jeshi hilo pia lipo tayari kukabiliana na machafuko ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na uchochezi huo.

"Ndani ya nchi yetu kwa kushirikiana na vyombo vingine tutawalinda wananchi na mali zao, tutakabiliana na matishio ndani ya nchi yetu, na sasa hivi tunaendelea kufuatilia kauli tata zinazoashiria uchochezi na machafuko ndani ya nchi yetu" amesema Jenerali Mabeyo

Kauli hiyo ya Jenerali Mabeyo ameitoa leo Jumamosi April 13, 2019 wakati wa hafla ya uzinduzi wa mji wa kiserikali uliojengwa Ihumwa mkoani Dodoman ambao unakusudiwa kunaziduliwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Mabeyo amesema kwasasa hali ya nchi ni shwari ila jeshi linaendelea kuimarisha ulinzi wa wananchi na mali zao kuhakikisha amani inaendelea kutawala. “Hali ya usalama kwenye mipaka yetu ni shwari, ndani ya nchi yetu JWTZ kwa kushirikiana na vyombo vya wengine liko tayari kuwalinda wananchi na mali zao, wakati wote tupo tayari kukabiliana na matishio yoyote yanayojitokeza," amesema.

Aidha Jenerali Mabeyo amezungumzia kuhusu ujenzi huo na kusema kwa kiasi kikubwa kazi hiyo imefanywa na vijana wa JKT na imefanyika kwa miezi mitano. Amesema kwa kuwatumia vijana hao, Serikali imeokoa takribani Sh2.1 bilioni, huku akieleza kazi yote hiyo imefanyika kwa Sh5 bilioni. “Mheshimiwa Rais vijana hawa wamefanya kazi kubwa sana, naomba kwa ridhaa yako utoe neno lolote la kuwafariji ila kwa upande wa maofisa