- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MKUU WA MAJESHI AAMUA KUTUA NJOMBE, ATOA YA MOYONI MAUWAJI YA WATOTO
Njombe: Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Nchini Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo ameamua kuweka kambi mkoani Njombe kufuatilia karibu matukio ya utekaji na mauaji ya watoto yanayo endelea mkoani hapo ambapo mpaka sasa kwa mujibu wa Kauli ya Waziri mkuu Kassim Majaliwa Idadi imefika 29.
Amesema amefika Njombe kwa kuwa yeye ni mwenyekiti wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama nchini Tanzania hivyo katika matukio hayo vyombo vyote vinashirikiana. Leo asubuhi Jumatatu Februari 11, 2019 amefanya kikao cha ndani na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Njombe pamoja na vikosi maalumu vilivyopo mkoani humo kuchunguza matukio hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mabeyo amesema sababu za utekaji na mauaji ya watoto yanahusisha zaidi ngazi ya familia na vyombo vya ulinzi na usalama vimeanza kuchukua hatua kukomesha mauaji hayo. “Vyombo vyote vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kwa kushirikiana pamoja na jeshi. Na mimi ndiye mwenyekiti wa vyombo vyote vya ulinzi hivyo ninaowajibu na si kwamba jeshi limeingia sasa, hapana hatujafikia hatua ya kuingiza jeshi,” amesema Mabeyo.
"Wananchi karibu nchi nzima wamesikia kinachoendelea Njombe. Wengine yamewatia hofu lakini si Tanzania tu mpaka nje ya mipaka yetu taarifa zimesambaa,” amesema. Ameongeza, “Sisi kamati ya ulinzi na usalama baada ya matukio tulileta timu maalumu mapema ishirikiane na vyombo vilivyopo huku (Njombe) katika kufanya uchunguzi makini na wa kina.”