- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MKUU WA JESHI LA ALGERIA AWASIFU WAANDAMANAJI NCHINI HUMO
Mkuu wa Majeshi nchini Algeria Luteni Jenerali Ahmed Gaed Salah amesema maandamano yaliyofanyika kwa muda wa mwezi mmoja nchini humo dhidi ya Rais Abdelaziz Bouteflika yameacha alama Kubwa na nimazuri yanayoonesha malengo muhimu na nia safi ya watu wa Algeria ambao wameelezea wazi maadili na kanuni za kazi ya kweli na kujitolea kwa ajili ya taifa lao, Hatua hiyo ni ishara kwamba jeshi hilo linaanza kujitenga na kiongozi huyo aliyetawala kwa muda mrefu
Hayo yanajiri wakati ambapo chama kimoja kati ya vinavyounda serikali ya muungano inayotawala nchini Algeria kimejitenga na Bouteflika.
Chama hicho cha National Rally for Democracy, RND ambacho kina ushawishi mkubwa na kilichokuwa kikimuunga mkono Rais Bouteflika kwa muda mrefu, kimemkosoa kiongozi huyo kwa kutaka kuendelea kubakia madarakani. Msemaji wa RND, Seddik Chihab amekiambia kituo cha televisheni cha El Bilad kuwa hatua ya kumuidhinisha Bouteflika kuwa mgombea wa urais wa awamu ya tano, ilikuwa ni kosa kubwa sana.