- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MKUTANO WA MBOWE WAVAMIWA NA VIJANA TAKRIBANI 50
Hai. Mkutano wa Mbunge wa Hai (Chadema) mkoani Kilimanjaro, Freeman Mbowe Umevamiwa na kuvurungwa na vijana takribani 50 wakike na wakiume wasiojulika walikotoka, mkutano huo uliokuwa ukifanyika katika kijiji cha Kikafu Chini, Kata ya Weruweru.
Mbowe alipanda jukwaani leo Jumanne Machi 3, 2020 saa 11:12 jioni ambapo alizungumza hadi saa 11:47 jioni ndipo kundi la vijana lilipoibuka na kuanza kupiga kelele, jambo lililomfanya mbunge huyo kunyamaza.
Hata hivyo kabla ya kunyamaza, Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alisema polisi hili ndilo kundi ambalo tuliwaambia na baada ya kauli hiyo alinyamaza akiangalia vurugu hizo.
Vijana hao wanaodaiwa kutoka maeneo mbalimbali walianza kupiga kelele wakisema "sema ulichofanya, tunataka Magufuli” hali ambayo iliwafanya polisi kuingilia kati kuanza kutuliza vurugu hizo. Baada vurugu kuendelea, polisi ambao walikuwa na gari moja waliongeza nguvu kwa kuja polisi waliokuwa wamevalia sare na kudhibiti kikundi hicho kusogelea jukwaa alilokuwa amesimama Mbowe.
Alivyonyamaza zaidi ya dakika 20 akiwatizama pasina kuongea chochote polisi nao walisimama ili wasiende kwenye jukwaa alilokuwa Mbowe wananchi walikuwa wakipa kelele. Baadaye waliondoka pasina kukamatwa. Walipoondoka vijana hao, Mbowe alishuka jukwaani na kupanda gari lake kisha kuondoka.
Awali, kabla ya Mbowe kupanda jukwaani, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Hai, Saimon Mnyampanda alidai kuna vijana zaidi ya 70 wa kike na kiume wametumwa katika mkutano huo ili kufanya vurugu. "Polisi kama ninyi hamtambui, sisi tunatambua, wapo vijana hapa wametumwa kutoka Kiungi, Bomang'ombe na wengine wa hapa, kufanya vurugu, tunatambua hilo," alisema Mnyampanda.