Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 7:43 pm

NEWS: MKURUNGEZI WA MANISPAA YA DODOMA ATANGAZA KIAMA KWA WALIOVAMIA MAENEO

DODOMA: MKURUGENZI wa Manispaa ya Dodoma,Godwin Kunambi ametangaza hali ya hatari kwa wananchi wote waliojenga nyumba zao katika maeneo ambayo siyo rasmi na kueleza kuwa nyumba hizo zitavunjwa.

Kunambi katoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na wamiliki wa nyumba katika manispaa ya Dodoma huku akisisitiza kuwa Dodoma lazima iwe na sura halisi ya makao makuu.

Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari ya Makole katika manispaa ya Dodoma,Kunambi alisema kuwa wapo watu waliojenga nyumba katika maeneo ambayo siyo rasini na kueleza kuwa nyumba jizo zitavunjwa.

Alisema kwamba wapo watu ambao walivamia maeneo ya wazi.hifadhi za barabara na wengine kujitwalia maeneo kinyume na taratibu na sheria jambo ambalo haliwezi kukubalika na hatimaye watu wa aina hiyo wataula wa chuya.

Kunambi ambaye alijinasibu kwa madai kuwa yeye ni mtu wa sura tatu alisema kuwa yeye ana sura ya kijikana maisha yake kwa maana ya kutojipendelea,kumpendelea mtu na kuhakikisha anatenda haki.

Mkurugenzi huyo alisema baada ya kuvunjwa kwa iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu(CDA) kuna changamoto nyingi ambazo zinatakiwa kutatuliwa bila kuwa na upendeleo huku sheria ikichukua mkondo wake.

“Mimi nataka kuwaeleza ndugu zangu namshukuru Mungu kwa kuwa nina sura tatu,sura ya kwanza ni kujikana,sura ya pili kutombendelea mtu na sura ya tatu ni kuhakikisha natenda haki,kwa maana hiyo sitamuonea mtu aibu pale ambapo atakuwa ametenda kinyume na sheria.

“Wapo watu ambao wamevamia maeneo ya watu,wapo watu ambao wamevamia maeneo ya hifadhi ya barabara,wapo watu ambao wamejenga maeneo ya wazi hao wote lazima watavunjiwa nyumba zao na siyo kuwavunjia bali watapewa NOTS ili waweze kuvunja wenyewe na wakishindwa watavunjiwa na kulipa gharama za uvunjaji” alisema Kunambi.

Katika hatua nyingine aliwashukia wenyeviti wa mitaa ambao wamekuwa wakihusika katika uuzaji wa viwanja kuholele na kusababisha madhara au migogoro kwa jamii ambayo ipo sehemu husika.

Alisema halmashauri haitawavumilia viongozi ambao siyo waaminifu ambao walishiriki au wanashiriki katika kuuza maeneo ambayo si rasm na kusababisha migogoro ambayo si ya msingi.

Hata hivyo kawataka wenyenyumba kuhakikisha wanawasimamia wapangaji wao katika suala zima la safi kwani kwa sasa mji wa Dodoma mbali kuwa makao makuu kunaelekea kuwa jiji hivyo usafi ni jambo muhimu kuzingatiwa.

Akizungumzia suala la wataalamu katika maispaa hiyo aliwataka wananchi wazitumie ofisi za Manispaa kwa kupitia vitengo tofauti tofauti badala ya kutumia muda mwingi kwenda kuonana na mkurungenzi kwani ofisi ya mkurugenzi ina kazi nyingi za kufanya.

Alisema wataalamu wake kila kitengo wako vizuri na wanafanya kazi kwa timu moja hivyo hakuna sababu ya kuvuka ofisi katika kitengo husika.

Kwa upande wa wamiliki wa nyumba wameishauri Manispaa kuwa wepesi katika kutatua matatizo pale ambapo yanapojitokeza hususani katika masuala ya mipaka ambayo wakati mwingine yamekuwa yakisababisha migongano.