- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MKURUNGEZI MKUU WA KAMPUNI YA NDEGE YA BOEING AJIUZULU
Mkurungezi mkuu wa Kampuni ya ndege ya Boeing Dennis Muilenburg ametangaza kujiuzulu kufuatia matatizo ya hivi karibuni yalioikumba Kampuni hiyo baada ya ndege za Boeing Max 737 kuaa na Hitilafu za Kiufundi.
Bodi ya wakurngezi ya kampuni hiyo imesema leo Desemba 23, 2019 kuwa Dennis Muilenburg anapaswa aachie ngazi haraka iwezekanavyo
Mwenyekiti wa Kampuni hiyo David Calhoun atakuwa Rais na Mkurungezi Mkuu mwezi Januari 13, 2020.
Dennis Muilenburg
Bodi hiyo imesema kuwa kubadilisha uwongozi kwasasa ni muhimu ili kuleta imani tena kwa wadau na wawekezaji
Ndege aina ya Boeing 737 iliyokuwa na abiria 149 na wafanyakazi 8 iliruka mwendo wa saa 8.38 za asubuhi kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole na kupoteza mawasiliano dakika chache baadae kwa mujibu wa shirika hilo la ndege la Ethiopia.
Utengenezaji wa ndege hizo ulikuwa ukiendelea licha ya ndege za chapa hiyo kuzuiwa kupaa kwa mezi tisa baada ya kuhusika katika ajali mbili zilizosababisha vifo vya mamia ya watu.
Zaidi ya watu 300 walipoteza maisha wakati ndege mbili za 737 Max zilipoanguka katika nchi za Indonesia na Ethiopia baada ya kuripoti matatizo katika mfumo wake mpya.
Boeing imekua ikitumaini kuwa ndege hizo zitarejea tena angani kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Hata hivyo wasimamizi wa safari za anga nchini Marekani wamesema wazi kuwa ndege hizo hazitapewa kibali cha kurejea angani katika siku za hivi karibuni.
Kampuni ya Boeing, yenye makao yake Seattle, Washington ni moja ya wauzaji wakubwa zaidi wa ndege duniani.
Kampuni hiyo imesema katika taarifa yake kwamba haitawafuta kazi wafanyakazi wanaofanya kazi na 737 Max, lakini kusimamishwa kwa utengenezaji zake kunaweza kuwaathiri wasambazaji na uchumi kwa ujumla.
"Kurejea kwa huduma salama za safari za 737 Max ni kipaumbele chetu cha juu," ilisema kampuni hiyo, "Tunafahamu mchakato wa huduma za 737 Max , masharti ya mafunzo yanayohitajika, lazima yatekelezwe kwa usahihi, kuhakikisha wasimamizi wetu, wateja na umma unaosafiri wana imani na 737 Max ."