- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MKURUGENZI WA ZAMANI WA KATANI AFARIKI AKIWA MAHABUSU
Mkurugenzi wa zamani wa Katani Limited Salum Shamte amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, alikokuwa akipatiwa matibabu, mkewe Mariamu Shamte amethibitish.
Mnamo Octoba 31, 2019 Shamte na Wenzake walifikishwa mahakamani wakikabiliwa na Makosa ya Uhujumu Uchumi na Utakatishaji wa fedha. Wenzake katika kesi hiyo ni Juma Shamte ambaye ni mkurugenzi wa sasa wa kampuni hiyo na mjumbe wa bodi ya Katani, Fatma Diwani.
Mashtaka yanayowakabili ni uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kusababisha hasara ya Sh1.14 bilioni kwa vyama vya msingi vya ushirika (Amcos)
Oktoba 25, 2019 Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) ilimteua Angelina Ngalula kuwa kaimu mwenyekiti wa taasisi hiyo wakati taratibu za kisheria zikiendelea kufanyika dhidi ya mwenyekiti wake, Salum Shamte ambaye siku hiyo alikuwa amefikisha takribani siku 10 polisi.
Shamte alikamatwa mkoani Tanga wiki iliyopita kwa tuhuma za kuhusika kwenye upotevu wa Sh54 bilioni zikiwemo fedha za Serikali kupitia kampuni ya Katani Limited ambayo inadaiwa ana maslahi nayo.