- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MKURUGENZI WA MANISPAA YA DODOMA AWATAKA WANANCHI WA DODOMA KUONDOA HOFU YA KUPATA HAKI
DODOMA: MANISPAA ya Dodoma imesema kuwa inaanza kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia,JOHN MAGUFULI ya kutaka wananchi wote wakiwemo wa Dodoma ambao walipewa hati za umiliki wa ardhi ya miaka 33 na CDA, waongezewe umiliki uwe miaka 99.
Hayo yameelezwa leo Mjini Dodoma na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma,GODWIN KUNAMBI wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Aidha amewatoa hofu wananchi ambao walipewa barua ya toleo yani Offer ya kiwanja na iliyokuwa Mamlaka ya ustawishaji Wa makao makuu, Kumbi amewata wananchi kuhifadhi vizuri risti zao vizuri kwani haki yao ipo hivyo wasiwe na wasiwasi kwani wao wapo kwaajili ya kuwatumikia wananchi.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo amewataka wale wote ambao wanamiliki eneo zaidi ya moja na hawajayaendeleza kwa muda wa miaka mitatu kwamba hawatawavumilia bali watawapokonya na kuwapa wengine ambao watakuwa na uwezo wa kuwekeza .
Pia amewatahadharisha wakazi wa Dodoma kufuata utaratibu katika kujenga hivyo hawataruhusu ujenzi holela.