Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 8:44 pm

NEWS: MKURUGENZI KORTINI KWA UHUJUMU UCHUMI

Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) imemkamata mfanyabiashara na mkurugenzi wa kampuni ya Zenon Oil and Gas Limited, Florencia Mashauri kwa tuhuma za wizi, uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.Dar es Salaam.

Pia amekutwa na kosa la ukiukaji wa sheria ya mafuta kwa kujenga kituo na kuiuzia mafuta kampuni ya usafirishaji ya Udart. Mashauri ni mke wa mfanyabiashara Robert Kisena ambaye naye ana kesi ya uhujumu uchumi.

Kaimu Mkurugenzi wa Uchunguzi Takukuru, Kassim Ephrahim amewaeleza waandishi wa habari leo Aprili 10, 2019 kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa jana na atafikishwa mahakamani leo.

Amesema katika uchunguzi wa Takukuru imebainika kuwa licha ya kampuni hiyo kusajiliwa kuingiza mafuta kwa wingi, haikuwahi kuagiza mafuta hayo na badala yake ilikuwa ikijihusisha na uuzaji wa petroli na dizeli kwa rejareja kwa kampuni ya Udart. Ephrahim ameeleza kuwa chini ya utaratibu huo kampuni ya Zenon iliiuzia Udart mafuta hewa na kuisababishia hasara ya zaidi ya Sh1.2 bilioni. Sambamba na hilo, Mashauri pia amekutwa na makosa mengine ambayo yameisababishia Udart hasara ya Sh2.4 bilioni.