- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MKURUGENZI JAMII FORUM AHUKUMIWA MWAKA MOJA JELA
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam nchini Tanzania imemuhukumu Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forum Maxence Melo kifungo cha kwaka mmoja jela au kulipa faini ya Sh. Milioni tatu(3) baada ya kupatikana na hatia katika kosa moja la kuzuia jeshi la polisi kufanya kazi yao ya uchunguzi kwa kuzuia taarifa binafsi za wateja wa mtandao wao wa Jamii Forum.
Hukumu hiyo imesomwa leo Aprili 8,2020 na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya kumkuta na hati Mshtakiwa huyo na moja.
Aidha mahakama imemuachia huru mshtakiwa Micke William ambaye ni Mwanahisa wa mtandao wa Jamii Forum, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake yakuwa ni mmoja ya wakurugenzi wa mtando huo.
Mshtakiwa Maxence Mello ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Kijamii wa Jamii Forum akipelekwa chini ya ulinzi baada ya Hakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumkuta na hatia katika kosa la kuzuia jeshi la polisi kufanya kazi yao ambapo amehukumiwa kulipa faini ya Sh. Milioni tatu ama kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani.
"Baada ya mahakama kupitia ushahidi wote tumejiridhisha kuwa mshitakiwa wa wapili Micke hahusiki Katika Kesi hiyo kwa namna yoyote ile, "Mshitakiwa huyo Katika utetezi wake alikanusha Mashitaka na kudai kuwa hata siku moja hakuwahi kuwa mmoja wa Wakurugenzi JamiiForums" alisema Hakimu Thomas
Mshtakiwa Maxence Melo wa kwanza kulia, Micke William katikati na wakili wa kujitegeme Nashony Nkungu wakiwa wamesimama nje ya ukumbi wa mahakama ha Hakimu Mkazi Kisutu kabla ya kusomewa hukumu yao