Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:49 am

NEWS: MKURUGENZI ATCL AWASHANGAA WANAOHOJI ITILAFU NDEGE AIR TANZANIA

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Ladslaus Matindi leo ametolea ufafanuzi ndege ya shirika la ndege la ATCL aina Bombardier Q400 iliyokuwa katika matengenezo, kwamba imeanza kufanya safari zake kama kawaida.

Image result for Ladislaus Matindi ATCL

Ufafanuzi huo ameutoa leo Jumatano Agosti 21, 2019 wakati akifanyiwa mahojiano na chombo kimoja cha habari nchini Tanzania cha Cloudsfm kupitia kipindi cha Power Breakfast baada ya jana kusambaa kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha picha ya ndege hiyo ikiwa katika matengenezo visiwani Zanzibar.

Aidha Matindi amesema ndege hiyo ilikuwa na hitilafu na ilitengenezwa kwa siku moja na tayari imerejea katika ratiba zake za safari za kila siku. “Ndege inaweza kuharibika, kupata hitilafu au kuingiliwa na kitu kutoka nje muda wowote kwakuwa ni mashine hakuna namna ya kuzuia hilo ni jambo la kawaida kwa mashine hata binadamu,” amesema Matindi.

Image result for Ladislaus Matindi ATCL

Amesema ndege hiyo ipo Dar es Saalam tangu jana na matengenezo yake yalichukua siku moja, akibainisha kuwa yalianza Jumatatu mchana hadi jana mchana,

“Usiku jana iliruka kurudi Dar es Salaam.” “Ndege zinazoharibika sio za ATCL pekee bali popote hata KLM ndege zao huwa zinaharibika, British Airways na Emirates wakisema ndege zao hazijawahi kuharibika ndipo tujiulize kwa nini zetu ziharibike.” amesema Mtindi.