- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MKE WA RAIS MANDELA AIZULU WILAYA YA BAHI, DODOMA
DODOMA: RAIS mstaafu wa nchini Ireland Mh.Mary Robinson pamoja na mke wa Rais mstaafu wa Africa Kusini Hayati Nelson Mandela,Mama Graca Machel wamefanya ziara ya siku moja Mkoani Dodoa kwa lengo la kuipa nguvu Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha kunakuwa na uwekezaji na huduma za Afya zinaboreka nchini.
Katika ziara hiyo viongozi hao wametembelea Zahanati ya Mpamatwa Wilayani Bahi ambapo Mh.Robinson amesema mabadiliko yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ni kichocheo kikubwa cha wao kufika nchini na kuwa wanatambua kushuka kwa bei za dawa na hiyo ni katika hatua za kuhakikisha huduma za Afya zinawafikia wanachi wa hali zote
Kwa upande wake Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia wazee na watoto Mh.Ummy Mwalimu amewasisitiza wananchi kujiunga na Mifuko ya Bima za Afya ili kuwa na uhakika wakupata matibabu kwa wakati wowote
Akiwasilisha taarifa ya hali halisi ya uzazi kwa akina mama,Mratibu wa huduma Ya Afya ya uzazi na mtoto Mkoani Dodoma Mary Shadrack yeye ameelezea baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta ya Afya mkoani hapa
Hata hivyo pamoja na baadhi ya wanachi kupongeza huduma za Afya wanazopatiwa pia wameelezea suala la kutakiwa kuchangia fedha katika huduma hiyo ili hali wanabima za Afya
Viongozi hao wastaafu ni wawakilishi wa Taasisi ya The Elders nchini Uingereza iliyoanzishwa na Hayati Nelson Mandela ikiwa na lengo la kushughulikia masuala ya Amani,Haki za Binadamu na huduma za Afya ambayo kwa sasa ipo chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa Ndugu Kofi Annan