- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MJUMBE WA CHAMA CHA KIKOMOSTI VIETNAM ATUA DOM
DODOMA: MJUMBE wa kamati kuu ya chama cha kikomonisti kutoka Vietnam, Chauvan Lam Aliwasili jana mjini Dodoma kwa lengo la kufanya mazungumzo na Chama cha Mapinduzi( CCM).
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kufanyika mazungumzao kati ya vyama hivyo Katibu wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi [NEC] Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, amesema lengo la mjumbe huyo kuwasili nchini ni kujenga ushirikiano na mahusiano ya kiuchumi kati ya CCM na chama cha kikomonisti.
‘’Lakini kusudi kubwa la ziara hii ni kuongeza ushirikiano na mshikamano ulikuwepo kati ya chama cha kikomosti na chama cha mapinduzi’’ amesema.
‘’Wote mnajua historia ya Tanzania tumeshiriki sana katika suala zima la ukombozi wa dunia kama mnavyojua Vietnam ilitawaliwabaada wakaja kujikombo kwahiyo kusudio kubwakuleta mahusiano ya karibu ya kiitikadi na kujengaushirikiano mzuri ndani ya taifana serikali kwa ajili ya biashara’’ amesema Lubinga
‘’ Kwamba vyama vyetu ni vyama rafiki na vyenye nguvu kwa hiyo wanataka tuendeleze urafiki huo mpaka siku za usoni’’amesema.
Akizungumzia suala zima la uchanguzi amesema mjumbe amewataka kuendeleza uchanguzi huo ili kutengeneza uhusiano wa karibu na kuongeza urafiki wao.
‘’Uchanguzi tukiumaliza uwe ni mwendelezo wa kutengeneza urafiki wa karibu licha ya huu wa kiuitikadi pamoja na uhusiano wa karibu wa kiuchumi na wao ndiyo maana tumeamua kuawaleta Dodoma ambapo wanakuta tunautaratibu wetu wakuchambua na kuchuja na walioomba nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama’’ amesema
Katika msafara huo mjumbe huyo aliongozana na wafanyabiashara pamoja na watalii licha ya kuwa hawakuweza kufika wote mjini hapa.