Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 9:54 am

NEWS: MJI WA TEXAS WAENDELEA KUTEKETEA NA MVUA

Texas: Mafuriko mapya yameripotiwa katika mpaka wa jimbo la Texas na Louisiana nchini Marekani kutokana na mvua kubwa inayoambatana na upepo mkali kuendelea kushuhudiwa.

Watabiri wa hali ya hewa wanasema kuwa huenda mvua hii ikaendelea kwa uda mrefu baada ya kuanza Ijumaa iliyopita.

Hakuna kinachoendelea katika mji wa Houston, ambao umebaki bila watu huku maji yakielea kila mahali.

Haya ndio mafuriko makubwa kuwahi kushuhudiiwa katika jimbo la Texas kwa kipindi cha miaka 50 sasa.

Watu 17 wamepoteza maisha katika janga hili la kiasili ambalo pia limesababisha hasara ya Mabilioni ya Dola za Marekani.

Inakadiriwa kuwa watu kufikia 50,000 wameathiriwa na mafuriko haya na kulazimika kuyakimbia makwao.

Rais Donald Trump aliwatembelea waathiriwa wa janga hili na kuahidi kuwa serikali yake itasawasaidia kujenga maisha yao upya.

Aidha, amewatia moyo na kuwaambia kuwa wao ni mashujaa.