Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 12:31 pm

NEWS: MIGOGORO YA NDOA YAONGEZEKA KWA 26%.

DAR ES SAALAM: Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya watoto Mwajuma Mwajuma amesema Kwa mujibu wa Takwimu za wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto za mwaka 2019 zinaonyesha migogoro ya ndoa imeongezeka kutoka migogoro 13,382 mwaka 2018 hadi kufikia migogoro 16,832 mwezi Juni 2019 sawa na ongezeko la asilimia 26%.

Amesema ongezeko hilo linatokana na mtawanyiko wa familia katika shughuli mbalimbali zinazowakabili wazazi na walezi ikiwemo pia wazazi kusahau wajibu wao.

Hayo yamebainika leo jijini Dar e salaam katika kongamano la kitaifa la waandishi wa habari kuhusu Agenda ya Kitaifa kuhusu wajibu wa wazazi/ walezi katika malezi na matunzo ya Familia liliwakutanisha wahariri na waandishi wa habari zinazohusu Watoto, Malezi na Matunzo ya Familia.


Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mtoto Mwajuma Magwiza amesema kuwa Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Wizara kwa kushirikiana na wadau kwa kipindi cha Disemba 2017 hadi Januari 2018 katika Halmashauri 12 za Ilala, Kinondoni, Temeke, Kigamboni, Ubungo, Arusha, Iringa, Mbeya jiji, Wilaya ya Mbeya, Dodoma, Nyamagana na Ilemela iligundua uwepo wa Jumla ya watoto 6,393 ikiwa watoto wa kike1,528 na watoto wa kiume4,865 wanaosihi na kufanya kazi mitaani.

Mwajuma Magwiza ameongeza kuwa kati yao watoto 1,385 watoto wa kike410 na watoto wa kiume 975 walitambuliwa wakiishi na kufanya kazi mitaani muda wa usiku uwepo wa watoto hawa maeneo ya mitaani kwa kiasi kikubwa unatokanana kutowajibika kwa familia katika kumudu majukumu yao ya kutunza na kulea watoto wao.

Aidha Mwamjuma ameongeza kuwa kulingana na Taarifa ya utafiti wa afya ya mama na mtoto na viashiria vya malaria ya mwaka 2015/16 inaonesha kwamba asilimia 25 ya kaya za mijini na asilimia 27 ya kaya za vijijini zina watoto ambao hawaishi na wazazi wao japokuwa mzazi mmoja au wote wawili bado wapo hai, hii inamaana wanaishi katika familia pana au wao wenyewe peke yao hivyo kukosa malezi ya wazazi wa pande zote mbili yaani baba na mama katika makuzi yao.


”Hii inawaathiri sana watoto kisaikolojia na wakati mwengine inasababisha na kuchangia kwa kiasi kikubwa watoto kuamua kuondoka na kwenda maeneo mengine ikiwemo mitaani, kujishughulisha na shughuli hatarishi kwa ajili ya kujipatia mahitaji yao.” amesema Mwajuma

Ameongeza kuwa kwa kuthamini na kutambua umuhimu wa Familia katika malezi na matunzo ya familia Serikali imendaaAjenda hiyo ya Kitaifa ambayo inalenga katika kuhakikisha kuwa wazazi na walezi na jamii kwa ujumla inakumbushwa na kuhimizwa kuwajibika katika kuwapa matunzo na malezi bora watoto kwa kuwajenga katika maadili, elimu ili waweze kufikia ndoto zao na kuwa na taifa bora.


“Niwaombe wamiliki wa vyombo vya habari kutenga muda wa kuwa na vipindi mahsusi vya kuwakumbusha na kuwaelimisha wazazi na walezi wajibu wao katika kuwalea, kuwatunza, kuzungumza na kuwapa upendo watoto ili kuhakikisha kuwa watoto wetu wanakuwa salama na kufikia ndoto zao na kuja kuwa wazazi bora wa baadae” amesema Mwajuma


Akizungumza kwa niaba ya katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Mkurugezi Msaidizi sehemu ya Familia kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Tausi Mwilima amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa familia inasimama imara na kutimiza wajibu wake katika kutoa malezi chanya Wizara imeandaa Ajenda hii ya Kitaifa ambayo inaweka msisitizo katika maeneo makuu 5 ambayo ni matunzo, ulinzi, mawasiliano, kujenga familia na upendo.

Maeneo hayo yakieleweka na kufanyiwa kazi watoto na vijana wetu watakuwa salama katika maeneo mbalimbali na tutaweza kutengeneza kizazi bora na imara chenye watu wenye maadili na uzalendo kwa Taifa letu.