- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MIAKA 30 JELA KWA KUMPA UJAUZOTO MWANAFUNZI FORMM 4
Kigoma. Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Kigoma imemuhukumu miaka 30 jela mkazi wa kata ya Mwanga manispaa ya Kigoma Ujiji, Isack Balayabala (25) baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya Sekondari Kaulananga.
Akisoma hukumu hiyo jana Ijumaa Agosti 16, 2019 hakimu wa mahakama hiyo, Eliya Baha amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo Desemba 2018 kwa kumpa ujauzito mwanafunzi huyo.
Katika kesi hiyo ya jinai namba 46 ya mwaka 2019 mahakama hiyo imesema imeridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.
“Kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 60A kifungu kidogo cha (3) cha sheria ya elimu namba 353 ya mwaka 2002 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016 kuwa mtu yeyote atakayempa mwanafunzi ujauzito atakuwa amevunja sheria na atahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.”
“Kutokana na ushahidi wa upande wa mlalamikaji uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi watano akiwepo aliyepewa ujauzito, baba wa mwanafunzi huyo, mwalimu mkuu katika shule aliyokuwa akisoma ,askari wa upelelezi na daktari wa hospitali aliyempima mahakama haina shaka na ushahidi huo, "amesema hakimu Baha.