- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MHARIRI MKUU WA GAZETI LA MAWIO ATISHIWA KUUWAWA
Dar es salaam: Mhariri mkuu wa gazeti la MAWIO lililofungiwa na Serikali juma lililopita baada ya kuchapisha habari iliyowahusisha maraisi wa zamani kwenye sakata la mikataba ya madini na makinikia amesema toka wakati huo amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka kwa watu wasiofahamika.
Tarehe 14 ya mwezi wa 6 Wizara ya habari nchini Tanzania ilitangaza kulifungia gazeti la kila wiki la MAWIO kwa muda wa miaka 2 kutokana na hatua yake ya mara kwa mara kuandika habari zinazoikosoa Serikali, ambapo liliandika habari iliyowataja maraisi wastaafu Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete kuhusika kwenye mikataba ya madini.
Uchunguzi wa hivi karibuni ulioagizwa na rais John Pombe Magufuli, umekadiria kuwa kiasi cha dola za Marekani bilioni 84 ambazo ni tozo za kodi zilipotea kutokana na makampuni hayo ya uchimbaji madini yaliyoanza toka mwaka 1998 kukwepa kodi lakini uchunguzi huu haukuwataja popote maraisi hao.Licha ya onyo lililotolewa na rais Magufuli, gazeti la MAWIO lilichapihs amaoni yaliyotolewa na mbunge wa upinzani Tundu Lissu, ambaye aliliambia bunge kuwa rais Kikwete na rais Mkapa wanahusika pakubwa na utata wa mikataba iliyotiwa saini katika kipindi cha mwaka 1995 hadi 2005 na 2005 hadi 2015 na kwamba walipaswa kuhojiwa na kamati zilizoundwa na rais.
Simon Mkina mhariri wa gazeti hilo ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP kuwa amekuwa akipokea vitisho vya simu kutoka kwa watu wasiofahamika toka gazeti lao lilipofungiwa.
“Baada ya gazeti kufungiwa, nimepokea takribani simu tatu za vitisho kwa maisha yangu. Niliuliza ninani aliyenipigia lakini alinikatia simu.
“Simu nilizopigia hazikuonesha namba. Kwahivyo nilishindwa kumpigia huyo mtu tena,” alisema muhariri huyo.
Mkina amesema kuwa tayari ametoa taarifa kwa bodi ya gazeti hilo pamoja na jeshi la Polisi ambalo limemjibu kuwa itakuwa vigumu kufanya uchunguzi kwakuwa simu zenyewe hazikuwa na namba.