- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MHANDISI LWENGE AWAONYA WATUMISHI WA UMMA KUHUSU UTII WA SHERIA.
Dodoma: Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi, Gerson Lwenge amesema njia nzuri ya kuondoa migogoro baina ya waajiri na waajiriwa ni kufanya majadiliano ya pamoja ambayo yameainishwa katika sheria ya utumishi wa umma Na. 9 ya Mwaka 2003 itakayosaidia kuongeza tija na kujenga nidhamu kwa watumishi kazini.
Mhandisi Lwenge amesema Watumishi wa Umma wanajukumu la kuhakikisha kuwa Maadili na Nidhamu katika utendaji kazi unakuwa chachu ya kuongeza ufanisi na utendaji kazi kwa kila mmoja .
Kiongozi huyo wakati akizindua baraza la tano la wafanyakazi wa mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira DUWASA, aliwataka waajiri kuzingatia sheria ya kazi na utumishi wa Umma.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira DUWASA Mhandisi, David Pallangyo na mwenyekiti wa Bodi ya DUWASA Balozi Job Lusinde,wakazungumzia baraza hilo.
Hata hivyo DUWASA imeiomba Wizara ya Maji na Umwagiliaji iendelee kuisaidia katika uwekezaji wa miradi ya majisafi na majitaka ili kukabiliana na ongezeko la mahitaji kutokana na uamuzi wa Serikali kuhamia DODOMA.