Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 4:16 pm

NEWS: MGOMBEA URAIS TUNISIA AFANYA KAMPENI GEREZANI

Mahakama ya Rufaa nchini Tunisia imefutilia mbali ombi la kuachiliwa huru Nabil Karoui lililotolewa na mawakili wake. Nabil Karoui ambaye amefuzu katika duru ya 1 ya uchaguzi wa urais nchini humo. Duru ya pili ya uchaguzi wa urais imepangwa kufanyika Oktoba 13 mwaka huu.

Nabil Karoui, ambaye ni mfanyabiashara maarifu nchini Tunisia, ameshitakiwa tangu mwaka 2017 kwa utakatishaji fedha na ukwepaji kodi.

Nabil Karoui hatashiriki katika kampeni ya uchaguzi wa wabunge. Wafuasi wake, pamoja na mkewe, Salwa Smaoui, wataendelea kunadi sera yake katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo, kama walivyofanya tangu mapema mwezi Septemba.

Kuna swali moja ambalo bado halijawekwa wazi: lile la kushiriki kwa mfanyabiashara huyo katika mijadala ya televisheni na mpinzani wake Kaïs Saeid kwa duru ya pili ya uchaguzi wa urais.

Uamuzi huu wa Mahakama ya Rufaa pia unaendelea kuzua wasiwasi kuhusu Nabil Karoui iwapo atashinda uchaguzi. Na uamuzi huo unaonekana kuwa utazua sintofahamu kuhusu uaminifu kwa matokeo ya uchaguzi, wadadisi wamesema.

Katika siku za hivi karibuni, chama chake, wapinzani wa kisiasa, waangalizi wa kimataifa walitoa wito wa kutaka Nabil Karoui aweze kufanya Kampeni kama wagombea wengine, bila mafanikio.