Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 5:29 pm

NEWS: MFANYABIASHARA KITANZINI KWA TUHUMA ZA KUBAKA

DODOMA: MFANYABIASHARA maarufu katika mtaa wa swaswa kata ya Ipagala Manispaa ya Dodoma Charles Kalinga maarufu Chaz Pub (43)amenusurika kifo baada
ya baadhi ya wakazi wa mtaa huo kumshushia kipigo Kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Dodoma wa kidato cha nne(17).

Tukio hilo lilitokea jana saa moja usiku katika mtaa wa swaswa baada ya mtoto huyo kusikika akipiga kelele akiwa katika pagale ambapo mama wa mtoto na majirani kumkuta mtuhumiwa akiwa amemlalia mtoto huyo huku akiwa ameisha muingilia kimwili.

Akizungumza na waandishi wa Habari mama wa mtoto hakiwa hospitali ya Mkoa alipokuwa amelazwa mtoto aliyebakwa,(Emy Mtunya) amesema mtoto huyo alitoka shuleni na kufika nyumbani ambapo alimuomba mama yake hela kwenda dukani kununua mahitaji.

"Nilianza kusikia kelele nikisikia sauti ya mwanangu akilia huku akisema mama nakufa,na sauti zilikuwa zikitokea katika pagare nilipofika katika pagare nilimuona Charles akiwa amemlalia mwanae huku akiwa tayari ameisha muingilia kimwili.

" Wakati huo mtuhumiwa aliuwa kavua suluali na mwanangu akiwa anavuja damu sehemu zake za siri,baada ya kumlazimisha kufanya tendo hilo baada ya kupiga kelele kwa lengo la kutaka msaada zaidi mtuhumiwa alikuwa akiniomba nisiendelee kupiga kelele na kudai kuwa anipatie kiasi cha laki moja ili aweze kukimbia.

“Wandelea na harakati za kunusuru maisha ya mwanangu wananchi wenye hasira kali walifika nyumbani na kuanza kumpiga Kalinga kwa kila aina ya kipigo huku watu wengine wakipiga polisi kwa lengo la kumnusuru mtuhumiwa huyo hadi polisi walipofikika kunusuru uhai wake” alisema mama wa mtoto.

Akizungumza wa mwaandishi wa habari mtoto aliyebakwa akiwa hospitalini akipatiwa matibanu amesema kuwa alibakwa na mtuhumiwa huyo kwa kumlazimisha huku akiwa amemshikia kisu na kumtishia kumuua iwapo atapiga kelele.

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Swaswa Robert Magelanga amekili kupokea taarifa za tukio la Charles Kalinga kumbaka mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondali Dodoma na kutoa taarifa polisi na kushikiliwa.

Naye kaimu Mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma, Caroline Damiani amesema majira ya jioni walimpokea Charles Kalinga akiwa amepigwa na alilazwa wodi namba moja na kuruhusiwa baada ya kupata nafuu na anaendelea vizuri.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma,Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea Kwa tukio hilo.

Amesema mtuhumiwa huyo mpaka sasa amekamatwa na jeshi la polisi kutokana na kuwepo kwa tuhuma za ubakaji ambazo zimedaiwa kufanywa kwa ubakaji huyo katika mtaa wa swaswa .