- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MEYA WA UBUNGO ACHACHAMAA KUONDOLEWA KWENYE NAFASI YAKE
Meya wa Manispaa ya Ubungo, jijini Dar es salaam Boniface Jacob amesema kwa mujibu wa Sheria na taratibu bado zinamtambua kuwa yeye ni Meya wa Manispaa hiyo.
Akiongea leo tarehe 8 Mei 2020, Mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Meya Jacob amesema mchakato uliotumika kumuondoa kwenye madaraka hayo, haukubaliki na ni haramu.
“Siku ya Jumamosi tarehe 2 Mei 2020, kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo aliutangazia umma, kwamba nimekosa sifa ya kuendelea kuwa Diwani wa Kata ya Ubungo na Mshatahiki Meya.
"Mkurugenzi kama afisa masuhuli na kiongozi mkubwa aliyeaminiwa na kuteuliwa katika ofisi ya umma alipaswa kufanya utafiti binafsi (Due diligence) kabla ya kufanyia kazi barua hiyo, kwa maana hiyo mtakubaliana na mimi hapawezi kuwa na utetezi kwamba Mkurugenzi hajui taratibu za Chadema kwa kuwa tayari taratibu hizo zilikuwa mezani kwake mwezi mmoja kabla" Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob
“Ni kwa kile kilichoitwa kuvuliwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), na mtu hewa. Asiyejulikana,” amesema Jacob.
"Walioratibu na kufanya uhuni huu ni mafisadi, majizi na wabadhilifu wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa kifupi itoshe kuwaita ni genge la wahalifu ambalo linatumia ofisi za umma kufanikisha adhima yao" Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Ubungo, Mhe Boniface Jacob
Amesisitiza, kwa kuwa taratibu za kuvuliwa umeya zilizoainisha hazikufuatwa, yeye bado ni meya wa Ubungo na kwamba, barua iliyotumiwa kumvua uanachama ni ya kughushi.
“Barua hiyo haikuwa na muhuri wa ofisi au sehemu inapotoka, haina mawasiliano ya ofisi au mtu aliyeiandika, haijanukuu vifungu vya vya Katiba ya Chadema,” amesema Jacob.
"Tumeandika barua kwa mamlaka za uchunguzi na mamlaka ya kinidhamu ya Mkurugenzi kufanyia kazi masuala mbalimbali kuhisna na kugushiwa kwa barua hiyo, kutumia jina la asiyehusika na asiye na mamlaka katika Chama na Mkurugenzi kufanyia kazi kinyume na taratibu, kanuni na sheria" amesema Meya Jacob
Jocob amesema kuwa, kitendo hicho kimetekelezwa na watu wenye nia ovu baada ya yeye na baadhi ya madiwani wa chama chake, kuanika hadharani upotevu fedha za Halmashauri kiasi cha shilingi 1.6 Bilioni. Jacob amesisitiza, kuwa taarifa zilizotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Beatrice Dominic hazina ukweli.