- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM AZUILIWA KUINGIA OFISINI KWAKE
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita leo Jumatatu Januari, 13 ameshindwa kuingia Ofisini kwake kuendelea na Majukumu yake ya Kila siku mara baada ya Ofisi ya Halmashauri ya Jiji hilo kubadilisha password ya mlango wa kuingilia ofisini kwa meya huyo kubadilishwa bila kupewa taarifa yeyote, kitendo ambacho kilichomfanya kulazimika kukaa njee ya Ofisi.
Baadhi ya hoja zilizotumiwa na madiwani wa CCM kumuondoa meya huyo wa upinzani ni pamoja na ile inayosema dereva wake alipata ajali kwa kutumia gari hiyo na pia mwenyewe alihusika na ubadhirifu wa takribani shilingi bilioni tano za umma - mambo ambayo anayakana.
Siku ya Januari 9, mwaka huu Meya huyo, Isaya Mwita, anayetoka chama kikuu cha upinzani cha Chadema, alitangazwa kuvuliwa wadhifa wake katika kikao kilichotawaliwa na vurugu, baada ya madiwani wa upinzani kudai kulikuwa na udanganyifu kwenye orodha ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Karemjee.
Mara baada ya hatua hiyo ya kumuondoa kufanyika, Meya Mwita alizungumza na waandishi wa habari kwa hisia kali, huku akiwataka viongozi wa dini kumwombea kutokana na yale anayopitia, na akiapa kupigania haki yake ya kuwa meya halali wa Dar es Salaam hadi dakika ya mwisho: "Bado mimi ni meya kwasababu kikao ambacho kimefanyika hapa kimepata dosari mbili ya kwanza tumepata changamoto ya udanganyifu wa jina la Mshamu aliye nje ya nchi, na mimi mara baada ya kufika hapa nilimueleza makamu kama mko na akidi mnaweza kuendelea, kumbe hawakuwa na akidi", alisema meya huyo.
Kulingana na hoja zake, kukosekana kwa akidi ya wajumbe waliopaswa kupiga kura ili aondolewe madarakani ndiyo sababu inayompa nguvu ya kupinga maamuzi ya kikao hicho na kufanya aendelee kujitambua bado ni meya. Ameapa kwenda mahakamani kutetea nafasi yake hiyo:
Imefahamika kuwa mara tu baada ya uamuzi huo kuchukuliwa na kikao cha madiwani 16 wa chama tawala cha Mapinduzi, CCM, Meya Mwita alinyang'anywa gari alilokuwa akitumia na pia ofisi yake ya umeya kufungwa.