- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MEYA WA IRINGA AONDOLEWA MADARAKANI
Meya wa Manispaa ya Iringa, (Chadema) Alex Kimbe ameondolewa kwenye Madaraka yake baada ya madiwani 14 kati ya 26 kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.
Meya huyo anakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na rasilimali za halmashauri, na kushiriki katika vitendo vya rushwa, sambamba na nidhamu mbaya kwa wafanyakazi wenzake.
Mkutano huo umefanyika leo Machi 28, 2020 katika Manispaa y Iringa, ambapo katika kikao hicho Madiwani 14 walikuwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku Madiwani 12 wakitoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Mara baada ya Kupigwa kwa kura hizo Meya Kimbe, amesema kuwa mchakato huo haujafata taratibu hivyo ataendela kuwa Meya wa Manispaa hiyo.
Jana Machi 27, 2020 MAHAKAMA ya hakimu mkazi Iringa iliondoa mahakamani hapo shauri dogo namba 5 la mwaka 2020 lililofikishwa katika mahakama hiyo na mstahiki meya huyo akipinga mchakato wa madiwani wa chama cha mapinduzi (CCM) kutaka kumung'oa katika nafasi yake ya umeya kwa tuhuma mbali mbali zikiwemo za matumizi mabaya ya madaraka