Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 10:01 am

NEWS: MEYA UBUNGO AACHIA NGAZI ATANGAZA KUTOGOMBEA TENA

Dar es Salaam. Meya wa Manispaa ya Ubungo, jijini Dar es salaam Boniface Jacob ametangaza uwamuzi wa kutogombea tena katika nafasi ya udiwani wa kata ya Ubungo katika uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2020.

Jacob ametangaza uamuzi huo leo April 6, 2020 kupitia mtandao wake wa Twitter akisema, “Nimetangaza kung'atuka katika udiwani kata ya Ubungo muda wa madiwani utakapo isha, sitogombea tena udiwani uchaguzi ujao..! Miaka 10 utumishi wangu ni kwa sababu Wana-Ubungo mlinikopesha imani. Tumekuwa wote wakati wa shida na raha, mabonde na milima.”


Hatua hiyo inakuja siku kadhaa baada ya wanachama zaidi ya 2000 wa chama chake cha Chadema kutia saini na kumfuata nyumbani kwake kumtaka agombee ubunge wa jimbo la Ubungo katika uchaguzi mkuu ujao 2020.

Akizungumza na kampuni ya Habari ya MCL Digital, meya huyo amesema hatua yake ya kutogombea nafasi ya udiwani ni hatua ya pili baada ya ile ya wananchi kutaka agombee ubunge wa Ubungo na sasa anakiachia chama kama kitampa ridhaa atafanya hivyo.

“Wale wananchi niliwakubalia kwa moyo mmoja lakini mimi sio final, sina maamuzi kuna ngazi kama tatu za chama za kumpitisha mtu kugombea ubunge, najua wananipenda sana ila niliwaomba wasubiri maamuzi ya chama.”