Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:30 pm

NEWS: MEMBE AMVAA ROSTAM AMTAKA AACHE KUZUNGUMZIA MAMBO BINAFSI

Dar es salaam: Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Njee na Ushirikiano wa Kimataifa nchi Bernard Membe amemtaka mfanyabishara na kada wa chama tawala ccm Rostam Azizi aachane na tabia ya kuzungumziz maswala ya binafsi (Persanl Issues) na badala yake ajikite kuzungumzia maswala Mapana ya nchi hasa yanahusu uchumi wa Tanzania.

Kauli hiyo ya Membe ameito leo Mei 17, 2019 muda mfupi baada ya kutoka mahakamani jijini Dar es Salaam ikiwa ni kama majibu kwa Rostam baada ya Jana Mei 16, 2019, picha moja ya video ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha Rostam akizungumzia suala la urais 2020 na kumshauri Membe asijitokeze kuwania nafasi hiyo badala yake aachiwe Rais John Magufuli kwa awamu nyingine.

Membe ambaye mwaka 2015 alijitosa kwenye mbio za kuwania urais, amesema Rostam hapaswi kuzungumzia mambo yanayomhusu mtu mmoja kwa sababu ya Taalumu yake.

“Napata kigugumizi mno kumjibu rafiki yangu Rostam, lakini Rostam ni mchumi na nitakutana naye nimshauri kuwa anafanya vizuri sana katika jamii ya Watanzania yanapozungumziwa masuala ya uchumi. Inabidi azungumze main issues za nchi, siyo personal, hizi tunaachia watu wa chini, level zetu ni kuzungumzia masuala ya kitaifa ya uchumi.

“Kwa level yetu ni kuzungumzia masuala ya kitaifa, kwa nini uchumi wetu upo hapa ulipo, kwa nini wafanyabiashara wanafunga biashara, huu ndio ushauri wangu kwake kwamba anafanya vizuri anavyojielekeza katika masuala ya uchumi,”

“Rostam ni mchumi hivyo angejikita katika eneo hilo kwa kuwa anafanya vizuri upande huo na asijaribu wewe ni mwenzetu sisi tumekatwa mkia, ukikatwa mkia hata ujitahidi vipi mkia wako utabaki kuwa mfupi. Tuwe tunazungumza kwenye dhamira zetu yawe sawa na yale tunayozungumza mdomoni, tuwe tunazungumza kitu ambacho binadamu watatuheshimu," amesema.