- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MDHAMINI WA LISSU ATAKA KUHAKIKISHIWA USALAMA WA MDHAMANA WAKE
Mdhamini wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, Ibrahim Ahmed, ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo kuwa mshtakiwa huyo amepona, ila ameshindwa kurudi nchini Tanzania kwa kuhofia usalama wake.
Ahmed ameieleza mahakama hiyo, leo Alhamisi Novemba 21,2019, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati wa kesi ya uchochezi inayomkabili mshtakiwa huyo na wenzake watatu ilipoitwa.
Lissu, aliyetarajiwa kurejea nyumbani mwezi Oktoba mwaka huu kwenye mahojiano na kituo cha habari cha VOA Swahili huko Washington, amedai kuna matamshi ambayo yamejitokeza kwenye mitandao ya kijamii kumtishia usalama wake.
Akizungumza kwa njia ya simu na kupitia runinga ya Chadema mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe katika makao makuu ya Chadema Lisu amesema kuwa atarudi nchini Tanzania siku hiyo ili kuadhimisha kushambuliwa kwake.
''Nitatua tarehe saba mwezi septemba 2019 kwenye ardhi ya tanzania kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa nitakuwepo, alisema Tundu Lissu
Tangazo hilo liliwafurahisha sana wanachama wa chama hicho waliokuwa katika makao makuu ya chama hicho.
Alitoa kauli hiyo katika andiko lake lenye kichwa cha habari kisemacho "Miaka Miwili ya Mateso, Matumaini".
"Nimeshakamilisha tiba kwa hiyo sababu ya kiafya ya kuendelea kukaa Ubelgiji haipo tena".
Septemba 7, 2017, Bwana Lissu alishambuliwa kwa silaha na watu wasiojulikana nje ya makazi yake Dodoma.
Toka wakati huo, Lissu na viongozi wengine wa upinzani wamekuwa wakilihusisha shambulio hilo na kazi yake ya siasa.
Wakati wa shambulio, Lissu hakuwa tu mnadhimu wa kambi rasmi bungeni Tanzania bali pia raisi wa chama cha wanasheria nchini humo.
Kwa kutumia kofia zake zote mbili, mwanasiasa huyo machachari alikuwa mwiba mkali wa ukusoaji wa serikali ya Magufuli.
Lissu alikuwa miongoni mwa wanansiasa wa upinzani waliopendelea kumuita Magufuli kuwa 'Dikteta Uchwara' ama kwa lugha ya kingereza'Petty Dictator'.
Baada ya shambulio hilo, alikimbizwa Nairobi kwa matibabu kisha Brussels Ubelgiji toka mwezi Januari mwaka 2018. Huko kote aliendelea kusisitiza kuwa serikali ya Magufuli ilikuwa na mkono kwenye shambulio dhidi yake.