- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MDEE, ESTER BULAYA NA MEYA UBUNGO WAFIKISHWA MAHAKAMANI
Dar es Salaam. Wabunge watatu wa Chama cha Upinzani nchini Tanzania Chadema, Halima Mdee, kutoka jimbo la Kawe, Ester Bulaya(Bunda Mjini) na Jesca Kishoa Viti maalum pamoja na Meya wa Ubungo, Boniface Jacob wamefikishwa katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu Machi 23, 2020.
Mara tu Baada ya kufikishwa mahakamani wamepelekwa katika mahabusu iliyopo mahakamani hapo kwa ajili ya taratibu nyingine.
Bado haijajulikana wanashtakiwa kwa makosa gani licha ya Kamnda wa polisi Kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa mnamo Machi 15, 2020 alizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa upelelezi dhidi ya wafuasi 27 wa Chadema wakiwemo viongozi wawili ambao ni mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Bunda mjini, Ester Bulaya wanaodaiwa kufanya fujo kutaka kuingia katika gereza la mahabusu la Segerea umekamilika na jalada litafikishwa kwa mwanasheria wa Serikali.
Mambosasa alidai kuwa Machi 13, 2020 mchana jeshi hilo lilipokea taarifa kutoka kwa maofisa wa gereza hilo kuwa kuna kundi la wafuasi wa Chadema limekusanyika katika geti la kuingilia gerezani hapo huku likiandamana na kufanya fujo.
Amesema wafuasi hao walifanya vurugu hizo walipokuwa wakienda kumtoa mwenyekiti wao Freeman Mbowe ambapo walikwenda kufanya vurugu kutaka kumtoa kabla ya kukamilisha taratibu.
“Tulifika eneo la tukio na kukuta askari wa magereza wakiendelea kuwadhibiti wanachama hao ndipo polisi walipowakamata watuhumiwa 27 na kuwapeleka katika kituo cha polisi Stakishari kwa mahojiano,” amesema.
“Baada ya mahojiano watuhumiwa wote 27 walidhaminiwa kwa mujibu wa sheria na watafikishwa mahakamani hivi karibuni kwani upelelezi wa shauri hili umeshakamilika,” ameongeza.