- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MCT YATANGAZA RIPOTI YA UVAMIZI WA STUDIO ZA CLOUDS TV
DAR ES SALAAM: Baraza la Habari Tanzania (MCT) limezindua Ripoti ya Hali ya Vyombo vya Habari hapa nchini kwa mwaka 2016 (State of the Media Report) ambapo ripoti hiyo hutolewa kila mwaka ili kuushirikisha umma.
Pia Baraza hilo linatoa ripoti kuhusu kuvamiwa kwa Studio za Clouds Media na kubaini jinsi tukio hilo lilivyoathiri uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa uhariri.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa Baraza hilo amesema ripoti hiyo haina lengo baya, bali ni kuweka bayana hali ya tasnia ya habari na kwamba Jambo hilo si mara ya kwanza kwani baraza hilo limekuwa likitoa ripoti kama hizo kila mwaka.
“Hatujafanya uchunguzi huu kwa kuwa tuna mapenzi na Clouds Media wala kwa sababu tuna mahusiano na Mkuu wa Mkoa, badala yake tumetoa ripoti hii kwa mujibu wa katiba ya MCT,” alisema katibu.