Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:48 pm

NEWS: MCHUNGAJI MWAMPOSA ACHILIWA KWA DHAMANA

Moshi. Jeshi la Polisi nchini Tanzania limewaachia kwa dhamana watu wanane akiwemo Mtume na Nabii, Boniface Mwamposa walioongoza kongamano lililosababisha vifo vya watu 20 mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.

Akizungumza leo Jumanne Februari 4, 2020 msemaji wa Jeshi la Polisi, David Miseme amesema baada ya kuachiwa kwa dhamana wataendelea kuripoti wakati uchunguzi ukiendelea.

“Watuhumiwa wanane waliokamatwa akiwemo Mwamposa, walihojiwa kwa kina na baada ya kujiridhisha, kupata yale yaliyokuwa yanahitajika katika uchunguzi wamepewa dhamana kwa mujibu wa sheria na wataendelea kuripoti wakati uchunguzi ukiendelea,” amesema Misime.

Amesema baada ya vifo hivyo vilivyotokea Februari Mosi, 2020 katika kongamano hilo,

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro alituma maofisa wakiwemo wataalamu wa uchunguzi wa sayansi ya jinai, kwenda kuungana na timu ya wataalamu Kilimanjaro

Amebainisha kuwa uchunguzi utakapokamilika, utatolewa kwa mamlaka husika na yatakayobainika yatatekelezwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu. Katika tukio hilo watu 20 walikufa, 16 kujeruhiwa. Leo majeruhi 14 wameruhusiwa kutoka Hospitali.