- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MCHUNGAJI MSIGWA AHOJI NAFASI YA SPIKA KUMSIMAMISHA MBUNGE
Dodoma. Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amehoji uhalali wa Spika wa Bunge Job Ndugai kumsimamisha Mbunge anayeliwakilisha Taifa kwenye Mabunge ya njee ya Tanzania pasi waliomchagua kuridhia
Akizungumza bungeni leo Ijumaa Mei 17, 2019 baada ya kuomba mwongozo kwa mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, Mchungaji Msigwa amesema uko wapi uhalali wa kiti cha spika kuwasimamishwa wawakilishi waliochaguliwa na chombo hicho cha kutunga sheria.
“Uhalali unatoka wapi na hawa hawakuteuliwa wamechaguliwa na nilitaka kujua anasimamishwa na kiti bila kujadili inatuchafua kama Taifa. Bunge litakuwa na nguvu gani ya kuwalinda hawa tunaowachagua,” amehoji Mchungaji Msigwa.
Ingawa Mchungaji Msigwa hakumtaja aliyekuwa akimlenga, lakini jana Alhamisi, Spika wa Bunge, Job Ndugai alitangaza kusimamisha uwakilishi wa mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele katika Bunge la PAP akimtuhumu kwa utovu wa nidhamu.
Ndugai alimtaka Masele ambaye ni makamu wa kwanza wa Rais wa PAP kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na kamati ya maadili ya CCM.
Akijibu mwongozo huo, Chenge amemtaka Mchungaji Msigwa kutowahisha hoja kwa maelezo kuwa tayari jana Alhamisi, Spika Job Ndugai alilitolea uamuzi kwa kuomba wabunge wasubiri taarifa itakapowasilishwa bungeni watakuwa na nafasi ya kujadili kwani milango haijafungwa.